Isaiah 59:13-15


13 aUasi na udanganyifu dhidi ya Bwana,
kumgeuzia Mungu wetu kisogo,
tukichochea udhalimu na maasi,
tukinena uongo ambao mioyo yetu imeuhifadhi.

14 bHivyo uadilifu umerudishwa nyuma,
nayo haki inasimama mbali,
kweli imejikwaa njiani,
uaminifu hauwezi kuingia.

15 cKweli haipatikani popote,
na yeyote aepukaye uovu huwa mawindo.

Bwana alitazama naye akachukizwa
kwamba hapakuwepo haki.
Copyright information for SwhKC